46. Twendeni Tumshukuru

1. Twendeni tumshukuru 

   na kumwimbia Mungu,

   aliyetupa roho 

   na nguvu mpaka leo.


2. Twaenda na kukua 

   miaka yetu yote.

   Hivyo mwaka kwa mwaka

   twafikia uzee.


3. Twaona shida nyingi, 

   uchungu na mateso 

   na vita na misiba 

   katika ulimwengu.


4. Kuhangaika kwetu 

   siku zote ni bure 

   asipotushikiza 

   Yeye atulindaye.


5. Na kama mama mwema ana

   vyomlinda mtoto 

   katika shida zote, 

   asipotee njia.


6. Hivyo na Mungu wetu 

   hulinda watu wake, 

   huwakingia shida, 

   huzuni na misiba.


7. Leo atuingiza 

   katika mwaka mpya, 

   hachoki kutupenda,

   kutufanyia mema.


8. Huruma zako ni mpya 

   kila panapokucha,

   hizo zinakomesha 

   uchungu wa mioyo.


9. Utubariki sote 

   katika njia zetu, 

   wakubwa kwa wadogo 

   wakalishe  mwangani.


10. U baba wa wakiwa, 

    u mshauri wa wajinga,

    u Mponya wa wagonjwa,  

    u msaada wa maskini.


11. Na mwisho twakuomba: 

    Utupe Roho wako,  

    atufundishe hapa, 

    atuongoze kwako.


12. Wewe mwenye uzima  

    utupe haya yote 

    sisi Wakristo wako!  

    Kwani twakungojea!

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya