47. Anza Siku Yako Hii

1. Anza siku yako hii kwa Jina la Yesu; 

   Mwombe akujalie, usimame naye.

   Kazi zako zote wee atazibariki.

   Na tena ulalapo, atakuwa kwako.


2. Asubuhi mapema 

   umwombe Mwokozi, 

   akusaidie Yee shidani popote.

   Atasimama kwako siku kuchwa pia, 

   na kumshinda Shetani akikujaribu.


3. Yesu akiwa nawe, waacha maadui, 

   usiogope hila zao zote mbaya. 

   Umtegemee Yesu, 

   shika mkono wake; 

   mtegemee Mwokozi, 

   Yeye atashinda.


4. Mambo yangu na shida

   ninakuwekea

   kama unavyopenda, zimalize zote.

   Kazi yangu nianze kwa Jina la Yesu 

   nakuomba: njoo kwangu, 

   unisaidie!


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya