48. Yesu Mponya tu Hapa

1. Yesu Mponya tu hapa, 

   moyo watulia,

   mawazo yetu yote

   uyavute kwako.

   Mwanga wa Neno lako, 

   utuangaze wote,

   tuwe na mwangazo.


2. Kaa karibu nasi, tunakutamani,

   mfunzi wetu ni wewe, 

   sisi wanafunzi. 

   Nenolo lina nguvu, 

   litatufanya wapya, laongoza vema.


3. Tuna furaha kubwa, tunakungojea.

   Wewe u mwamba wetu 

   tutegemeao. Bwana tunakushika

   mpaka tunapofika uzimani kwako.


4. Twataka utufunze kuwa na upole. 

   Tufanane na wewe unyenyekeavyo. 

   Utimizavyo kazi, ulivyofanya bidii 

   kuwa mpatanishi.


5. Nguvu ya Roho wako 

   ionyeshe kwetu, 

   unavyomulikia wanaopotea.

   Kwa kinywa chako Yesu 

   utushindie nasi, 

   tuwe wako kweli!

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya