5. Nikulakije Vema
1. Nikulakije vema
Bwana wangu Yesu?
Wote wanakungoja
wapewe uzima.
Nuru yako ing’aze
hata moyo wangu.
Nijue mambo mema,
yakupendezayo.
2. Wamekutandikia
maua na nguo.
Nami nakuimbia
nyimbo za furaha.
Moyo ukupendeze
kwa sifa na nyimbo
ukakutumikie
siku zangu zote.
3. Umetoka mbinguni
ukawa maskini.
Ukaacha furaha
utupe uzima.
Na tuliponyang’anywa ufalme
na raha,
ukaja Mponya wetu
kuturudishia.
4. Nalifungwa na mwovu:
Ukanifungua.
Nikawa nimetwezwa,
ukanitukuza.
Ukanifanya mkubwa,
ukanipa mali,
zisizomalizika,
kwa kutu na wezi
5. Umenijia mimi,
sababu ya nini?
Sababu ya kupenda,
uwaponye wote;
waonao huzuni,
kwa makosa yao,
wakijuta kwa kweli,
utawapokea
6. Ushike neno hili:
Umati wa Yesu,
ukiwa na huzuni,
na shida popote.
Usiogope kitu,
wokovu tayari.
Anayetufariji,
yu karibu sasa.
Comments
Post a Comment