50. Twapenda Ukaapo
1. Twapenda ukaapo
Bwana wetu enzini,
furaha zako wewe
zinazipita zote.
2. Palipo pa kuomba
wajapo watu wako
na wewe Bwana upo,
uwakubali wote.
3. Twapenda Neno lako,
habari za wokovu,
za nguvu za kushinda,
za shangwe za mbinguni.
4. Twapenda nyimbo zako,
tunaziimba hapa,
mpaka tutaziimba
pamoja na malaika.
5. Utujalie Yesu,
tuzidi kukupenda,
tuone uso wako
utakavyotakata.
Comments
Post a Comment