51. Yesu Ndiye Kiongozi Wangu

1. Yesu ndiye kiongozi wangu,

   kumfuata Yeye ni furaha, 

   ajuaye kuongoza vema, 

   anilinda, nisione shida,

   analeta raha moyoni.


2. Bwana Yesu akiniongoza, 

   nitapita pori na misitu, 

   nitavuka mito na bahari 

   kwa furaha, kwani nina njia

   ya kufika mjini kwa

   Mungu.


3. Nikilala Yesu anilinda, 

   anitunza Yeye siku zote. Hata 

   nikifika njia panda, nikiona

   shaka, aonyesha 

   njia ya kufikia kwake.


4. Siku zote namfuata Yeye,

   sitaona kiu wala njaa; 

   anitunza kwa rehema nyingi:

   nitaweka mikononi mwake

   moyo wangu, auokoe. 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya