52. Jina Lake Yesu Tamu
1. Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia.
Hutupoza, tena hamu
hutuondolea.
2. Roho iliyoumia
kwalo hutibika,
chakula njaani pia;
raha, tukichoka.
3. Jina hili ni msingi,
ngao, ngome, mwamba,
kwa hili napata wingi
kwangu ni akiba.
4. Yesu, Mchunga, Rafiki,
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.
5. Moyo wangu hauwezi
kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.
6. Na utakaponiita,
kuja kwako Bwana,
huko kwako sitaacha
kukusifu sana.
Comments
Post a Comment