55. Mmoja Ndiye

1. Mmoja ndiye tumpendaye,

   aliyetoa mwili wake 

   akikubali mateso.

   Twakupa mioyo yetu 

   Mwokozi uliyetufia, 

   twapenda kuwa wako tu. 

   Bwana tukubali! Ututengeneze 

   sisi wako. Nuru yako itung’aze 

   tusipotee gizani.


2. Sisi hatukukuita,

   ila umetuita wewe,

   huruma yako ni kubwa. 

   Nguvu zetu hazitoshi, 

   kukufanyia kazi njema 

   usipotutia nguvu.

   Shida yetu sisi ndio ulegevu,

   uondoe; nia zetu zigeuzwe 

   tufanye kazi kwa bidii.


3. Yesu, wewe umesema: 

   “Watenda kazi ni wachache 

    kwenye mavuno ya Bwana.”

    Twaomba: Tutume nasi, 

    tualike wageni wengi, 

    nyumba ya Bwana ijae.

    Heri watu wale uliochagua 

    kuja kwako kwenye raha

    na furaha, milele hata milele.


4. Uwahurumie watu

   walio mbali na wokovu

   wanaoshikwa na giza.

   Hawajasikia bado 

   utume mwema wa wokovu 

   tunaopewa na Mungu.

   Jua la uzima liche hata kwao. 

   Njoo Mwokozi! Tangulia! 

   Twafuata, Ukifungua  milango.


5. Tunataka kutangaza

   habari ya upendo wako, 

   ya moyo wako wa kweli. 

   Tutawaonyesha watu 

   msalaba wako siku zote,

   mpaka washindwe mioyoni.

   Kwani Neno lako 

   lina  nguvu kubwa ya kushinda.

   mzigo wako ni mwepesi.

   mlango wa mbingu ni wazi.

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya