56. Mmoja ni Mfalme
1.`Mmoja ni Mfalme
shujaa, ni mshindaji!
Enyi adui, kimbieni tu!
Nawe Sayuni uone furaha
ukapumzishe kabisa moyo:
Uzima, utengemano, furaha
ndizo Mwokozi atakazokupa.
2. Twende kuonja maji ya uzima
tunayopewa na Bwana Yesu,
aliyesema
“Njooni kwangu nyote,
nitapumzisha mioyo yenu.”
Nyweni, wapenzi, katika kisima
chenye wokovu
wa wenye huzuni.
3. Mfalme wa mbingu
ataka kuwapa
kilemba kizuri cha urembo,
awawekea vitu vya milele,
heshima hiyo ni ya kushinda.
Vumilieni taabu na shida:
Yesu mwenyewe ni tuzo la vita.
4. Nguvu, ujuzi, heshima na sifa
ni zake Mungu
na Mwana wake.
Nami nataka kufika mbinguni!
Nifunguliwe mafungo yangu!
Mwenye upendo atanisikia.
Wenye uzima wanamsifu
Mungu.
Comments
Post a Comment