57. Nani Mpenzi Wangu Mkuu?
1. Nani mpenzi wangu mkuu?
Nani ninayemsifu?
Nani ninayemjua?
Nani ninayempenda?
/:Ndiye Yesu Mwokozi.:/
2. Nani nimtegemee,
anipaye moyo mkuu?
Nani aondoaye,
makosa, shida zangu?
/:Ndiye Yesu Mwokozi.:/
3. Nani anayenipa,
nguvu nyingi za roho?
Nani anifanyaye,
mwenye haki kwa Mungu?
/:Ndiye Yesu Mwokozi.:/
4. Nani mwenye faraja,
nikiona huzuni?
Nani atulizaye,
moyo wenye taabu?
/:Ndiye Yesu Mwokozi.:/
5. Nani azishindaye,
hata nguvu za kufa?
Nani anipeleke,
baadaye kwake Mungu?
/:Ndiye Yesu Mwokozi.:/
Comments
Post a Comment