58. Jina Moja ni Kubwa sana

1. Jina moja ni kubwa sana:

   Ni Jina lako Bwanangu! Nasifu

   Jina hili lako, 

   Yesu Kristo u Mwokozi.

   Li tamu kwangu Jina hili,

   jina jingine silijui.


2. Naliandika Jina hili 

   rohoni mwangu kabisa. 

   Silisahau siku zote, 

   halifutiki moyoni.

   Li tamu kwangu Jina hili, jina 

   jingine sitafuti.


3. Jina hili ni jua langu 

   lawaka ndani ya roho.

   Lanipa na utengemano,

   lafuta makosa yote.

   Li tamu kwangu Jina hili, jina

   jingine sifahamu.  

   baadaye kwake Mungu?


4. Jina hili ni boma langu, 

   upanga wangu vitani,

   ni ngao yangu na silaha, 

   lamshinda hata Shetani.

   Li tamu kwangu Jina hili, jina

   jingine silitaki.


5. Jina hili lanipa nguvu, niweze

   kwenda kwa haki. Ujuzi wote

   umo humo  

   katika Jina la Yesu.

   Li tamu kwangu Jina hili, jina

   jingine sitamani.


6. Ee Yesu, Jina lako ndilo furaha

   yangu nikifa.

   Ni cheti cha kuingilia 

   mbinguni kwa Bwana 

   Mungu.

   Ndipo nitalisifu sana, 

   jina jingine silijui.

 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya