59. Kazi ni Yako Bwanangu
1. Kazi ni yako Bwanangu
tunayoifanya;
hakuna anayeweza
kuvunja kazi hii.
Ni kama punje ya mbegu
ikiwa ndani ya mchanga,
inakufa kwa kuoza;
na hapo yabadilika,
inaota, yakua na kuzaa.
2. Yesu, umeteswa kwanza,
halafu umepaa.
Nao wakufuatao
wanateswa vivyo.
Twaomba tusaidie
nasi tushike njia hii,
kwa kufa kwako na sisi
tunatoka kaburini.
Tuongoze, tufike mbinguni.
3. Bwana wewe umekufa
kwa ajili yetu.
Ukaweka ufufuo
ulipofufuka.
Twaomba: Tuma mitume,
wajulishe Jina lako
mpaka mwisho wa dunia.
Utukubali na sisi
kwa kazi hii, tutume,
twakutii!
Comments
Post a Comment