61. Sifuni Nyote Huruma
1. Sifuni nyote huruma ya
Mungu,
kwa nyimbo nzuri,
umati wa Yesu!
Atualika furahani:
/: Msifuni Bwana kwa
neema yake! :/
2. Yeye ni Mfalme
anayetawala;
viumbe vyote
vinamtumikia,
hata malaika
wamwabudu,
/: wanamwimbia kwa
sauti nzuri. :/
3. Enyi mataifa, hofu
iacheni!
Njooni kwa Yesu,
Mchunga kondoo
mwema.
Sikilizeni Neno lake:
/: Atukomboa kwa kufa
kwake.:/
4. Awapa watu chakula
chochote,
atushibisha kama baba
mzuri,
aleta jua hata mvua,
/: atubariki kwa wema
wake. :/
5. Sifuni nyote huruma ya
Mungu,
kwa nyimbo nzuri,
umati wa Yesu!
Sasa huzuni twaishinda:
/: Msifuni Bwana kwa
neema yake! :/
Comments
Post a Comment