62. Uamke Kwetu Tena Roho
1. Uamke kwetu tena Roho wa
mashahidi wale wa kwanza,
waliokesha siku zote,
waliomshinda yule adui,
wakihubiri Neno la Yesu
kwa watu wa ulimwengu wote.
2. Uwashe moto wa upendo,
uendelee pote kuwaka.
Peleka watu mavunoni,
wanaofanya kazi kwa bidii.
Bwana mwenye mavuno,
tazama:
Watenda kazi yako ni haba.
3. Mwanao ametuagiza kuomba
hivi kwa Jina lake,
na sisi wanafunzi wake,
twashika Neno lake kwa bidii.
Twaomba hivi kwa moyo wote.
Ee Bwana usikie, ufanye!
4. Utume watu wengi sana,
walitangaze Neno kwa nguvu.
Tusaidie, tuokoe;
ufalme wa Shetani uishe.
Usimamishe, Bwana wa
mbingu,
ufalme wako
ulimwenguni!
5. Utume mwema na uende
mahali popote huku nchini.
Wa dini zote waingie
kundini mwako mwa
wateule. Amsha nao Wana wa ahadi na
wa Imani zote wakutii.
Comments
Post a Comment