65. Yesu ni Mponya
1. Yesu ni Mponya, aleta furaha!
Mwanzo na mwisho
wa vyote ndiye.
Mwana Adamu
na Mungu wa kweli
ametujia atubariki.
Mbingu, dunia, toeni habari:
Yesu ni Mponya, aleta furaha!
2. Yesu ni Mponya, aleta wokovu!
Sikilizeni habari njema!
Sisi tulipomwacha Mungu wetu
akaturudisha tena kwake.
Ametufanya watoto wa Mungu.
Yesu ni Mponya, aleta wokovu.
3. Yesu ni Mponya, aleta uzima!
Kamba za kufa zimekatika.
Mwana wa Mungu
kumshinda Shetani,
awakomboe watumwa wake,
amewapata, kawapa uhuru.
Yesu ni Mponya, aleta uzima.
4. Yesu ni Mponya,
Mchungaji wa kweli,
anayelisha vizuri kondoo.
Wote walio mbali awaita,
awarudishe kundini mwake.
Awakomboa kondoo kufani:
Yesu ni Mponya
Mchungaji wa kweli.
5. Yesu ni Mponya
na Mfalme wa enzi!
Mbingu zimsifu na watu wamtii.
Anageuza mioyo ya watu, hata
na sisi tumpe yetu,
kwani apenda kutupa uzima.
Yesu ni Mponya
na Mfalme wa enzi!
6. Yesu ni Mponya
na mwenye upendo!
Anatupenda kwa moyo wote.
Yeye mwenyewe
upendo wa kweli,
aliyekufa kwa kutupenda.
Nasi tumpendaye
kwa nguvu ya roho!
Yesu ni mponya na
mwenye upendo.
Comments
Post a Comment