66. Mfalme ni Yesu Pekee
1. Mfalme ni Yesu pekee,
wote wanamwangukia,
watawalishwa na Mungu,
Ndimi zote ziungame
Yesu ni Mfalme wa pekee,
atukuzwe popote.
2. Mfalme mkubwa, watu wako
wakutii, wanakusifu.
Yesu apita wafalme,
Yeye ndiye mkubwa sana,
apenda kuwakomboa,
kwani ndiye Mwokozi.
3. Enyi watu mpeni mioyo,
mnaohuzunika njooni;
wakiwa semeni naye,
kwani vyote aviweza.
Awagawia uzima
wanaomngoja yeye.
4. Kama wataka uzima,
nenda kwake, acha soni,
Yeye anakungojea.
Amejitoa mwenyewe,
wewe upate kurithi,
mbingu ni yako sasa.
5. Nimsifuje Yesu Kristo
mimi vumbi, mimi jivu?
Nasema: Nitamtangaza
Kristo Yesu ndiye Bwana!
Na tumpende, tumheshimu
sifa zote zampasa.
Comments
Post a Comment