74. Bwana Uliyewaita Watakatifu
1. Bwana uliyewaita,
watakatifu wako,
wawe mitume, wachunga,
walishe kundi lako;
Wanyonge na wenye hofu
wakawa mashujaa,
na wapole wa kunena
wasiwe kunyamaa.
2. Hata leo wawataka
watakatifu wako,
nawe wauliza tena,
ni nani aliyeko atakaye
nimtume afundishe vijana?
Ni tayari, Bwana wangu,
Nitume mimi Bwana.
3. Nitume na mimi, Bwana,
kama ulivyotumwa,
habari ya msamaha,
na dhambi kutubiwa,
niwahubiri wakosa,
na waliopotea,
wokovu u wake Bwana,
aliyewafilia.
4. Astahiliye hapana
kutamka habari,
lakini Wewe waweza
kutufanya tayari
Neno lako tulijue,
tupe na Roho wako,
hayatakuwa ya bure,
haya maneno yako.
Comments
Post a Comment