1. Hosiana Mesiya, aingia mjini kwake. Fagieni popote, zipambeni njia zote; Tandikeni maua, aingie na shangwe. 2. Hosiana Mwokozi! Njoo, twakungojea Bwana Tumepamba mioyo, twakukaribisha kwetu. Tunakufungulia, milango ya mioyo 3. Hosiana, ee Shujaa! Utusaidie sisi. Tuwe wako kwa kweli, tukutumikie vema. Kwani hutakubali watu wasiokutii. 4. Hosiana Mfalme mkuu! Uingie kwetu hima! Uliyebarikiwa, Uingie mlango wetu. Hosiana, karibu! Bwana, njoo! Haleluya!
Comments
Post a Comment