78. Mwokozi Wangu Umekosa Nini?

1. Mwokozi wangu 

   umekosa nini?

   Wahukumiwa kama mwuaji.

   Umeshtakiwa makosa 

   mangapi uliyotenda?


2. Wapigwa sana, 

   miiba taji lako,

   umetemewa

   mate, watukanwa, 

   wanyweshwa nyongo 

   tena siki kali, 

   wasulibishwa.


3. Sababu gani 

   unateswa hivi? 

   Makosa yangu 

   yanakuumiza;

   mateso haya yako yanipasa,

   mimi mkosaji.


4. Ajabu kubwa 

   sana tendo lako; 

   Mchungaji unateswa kwa 

   ajili ya kondoo,

   Bwana 

   unawalipia watumwa wako.


5. Tulipokuwa mateka 

   wa mwovu,

   nawe ukaja ukatukomboa.

   Tulistahili kufa kwa 

   milele,

   ukatufia.


6. Mwokozi wangu

   nifanyeje mimi,

   niitangaze pote sifa yako? Na-

   kufuata nikutumikie 

   maisha yote.


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya