79. Nakusalimu Kichwa
1. Nakusalimu kichwa
kilichojaa damu,
kilichovikwa taji
la miiba mikubwa,
kilichopata enzi
kwa Mungu mbinguni,
kitukanwacho sasa
matusi makali.
2. Naona uso wako
watemewa mate,
heshima yako yote
imeondolewa.
Mwanga wa macho yako
wazimika sasa.
Aliyekuharibu hivi,
ndiye nani?
3. Mateso yako Bwana,
yanipasa mimi.
Wewe waadhibishwa
kwa ajili yangu.
Hukumu unapata
iliyonipasa.
Bwanangu nakuomba,
unihurumie!
4. Na mimi nasimama
msalabani pako;
niwe karibu kwako
utoapo roho;
ukiugua sana
kwa teso la kufa,
nitakushika Bwana
kwa moyo wa pendo.
5. Bwana nayashukuru
masumbuko yako,
sababu ya kuteswa
na kufa kuchungu.
Wewe umenishika,
nami nakushika,
kwa ajili yangu.
Hukumu unapata
iliyonipasa.
Bwanangu nakuomba,
unihurumie!
6. Moyo unaposhikwa
na woga wa kufa,
usiniache Bwana
katika vita hii.
Siku ya kufa kwangu
unisaidie,
kufa kwako kuchungu
kutaniokoa.
7. Niwie kama ngao
nitakapokufa,
nione uso wako katika uchungu.
Ndipo nikutazame
nikukumbatie!
Anaye kufa hivi
afa kwa amani.
Comments
Post a Comment