80. Liko Neno Moja Nipendalo

1. Liko Neno moja nipendalo, 

   ni chakula cha moyo;

   Neno hili linanituliza

   nikipatwa na shida: 

   Kumtazama Bwana wetu pale,

   atoapo jasho kama damu,

   akubalipo mzigo, 

   Baba aliomtwika.


2. Siku zote  namkumbuka  yeye, 

   alivyosulibishwa, 

   akivumilia taabu kimya 

   kama mwana wa kondoo.

   Nami akanikumbuka mimi,

   akisema: Yamemalizika! 

   Huko aliniteka,

   nami niwe mtu wake.


3. Bwana wangu, 

   u mwenye huruma, 

   mimi ni mkosaji tu; 

   nilipokuwapo penye giza

   wewe ukatokea, 

   ukamtafuta kondoo wako,

   kabla mimi sijakusikia.

   Watoa ukombozi unipao uhuru.


4. Ndimi huru lako, Bwana Yesu,

   wewe ndiwe Bwanangu. 

   Jina lako, bora liung’aze moyo 

   wangu vizuri.

   Amani yako nikae nayo, 

   siku zangu zote mpaka kufa.

   Ndivyo ninavyoomba, 

   Bwana unikubali. 


Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya