83. Yesu, Kuteswa Kwako
1. Yesu kuteswa kwako
nitakufikiri.
Nipe kwa shauri hili
roho na mbaraka.
Moyo wangu uone
hali yako Yesu,
jinsi ulivyoteswa
kwa ajili yetu.
2. Moyo wangu uone
taabu yako kubwa,
maumivu, mapigo,
na kuwambwa mtini,
taji lako la miiba
tena misumari,
iliyokuumiza,
hata kufa kwako.
3. Nikitazama yote
yaliyokutesa,
nifikiri sababu
na maana yake.
Sababu ndio mimi
na makosa yangu:
umepata mateso,
nipate huruma.
4. Yesu unifundishe
nijute kwa moyo;
nisikuzidishie
shida na uchungu.
Nisiweze kupenda
yaliyokutesa:
nataka kuyaacha
na kukufuata.
Comments
Post a Comment