87. Ee, Watoto Njooni
1. Ee, watoto njooni,
njooni Golgota,
mtazameni Yesu aumizwavyo!
2. Mtazameni huko
mkamtazame,
Sogeeni kwake, ametupenda.
3. Sogeeni kwake, mkamtazame,
mioyo iyeyuke, mwangukieni!
4. Mioyo imlilie anayeteswa;
mzigo wetu mkubwa aukubali.
5. Mzigo wa makosa
ya ulimwengu.
Mpeni nanyi nyote
mioyo yenu!
6. Apata mshahara, ni kufa kwake;
wewe una raha, kwake ni kufa.
7. Ataona enzi ya utukufu.
Tuimbe Haleluya
na kumshukuru.
Comments
Post a Comment