89. Kumbuka Getsemane

1. Kumbuka Getsemane, 

   asongapo Shetani, 

   Mwokozi ukamwone 

   ateswavyo shambani; 

   nao uchungu wewe, 

   aombapo kumbuka!


2. Kumbuka barazani

   ashtakiwapo Yesu; 

   mtazame Bwana huko,

   walipomhukumia; 

   upate soni wewe,

   mti wa Yesu kumbuka!


3. Kumbuka na Golgota 

   alipokufa Bwana.

   Upaji wa tambiko 

   ameutoa Yeye. 

   Kasema: Imekwisha

   Mti wa Yesu kumbuka!


4. Kumbuka bustanini 

   walipomzika Yesu, 

   kukiwa bado giza. 

   Mfu amekwenda wapi? 

   Amefufuka Yeye; 

   Ufufuko kumbuka! 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya