9. Faraja, Tumaini Langu

1. Faraja, tumaini langu 

   usiniache gizani.

   Moyo ni wazi kukungoja,

   Ee Yesu uniingie. 

   Furaha ya mbingu na

   nchi, Mwana Adamu na Mungu;

   Ee nuru kutoka mbinguni, an-

   gaza moyo wangu huu.


2. Mtoto mpendwa,

   nakuomba, chagua moyo

   wangu huu, ufanye kuwa hori

   lako ukalazwe humo wewe.

   Ili nipate mwisho mwema 

   wa shida yangu na vita. 

   Zaliwa ndani yangu Yesu,

   na ndani yangu ukue.


3. Mwokozi wangu utulize,

   tumaini hili kubwa.

   Ukija nitakupokea

   kwa roho nyenyekevu, hii.

   Uweza wangu wote

   pia wakungojea kwa 

   uchu. Nataka 

   kukutumikia:

   Njoo, Yesu usikawie. 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya