90. Mtini Mponya Alipowambwa
1. Mtini Mponya alipowambwa,
ndipo nimwombapo upozi
akaniokoa mpenzi.
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu
Mwokozi wangu.
Mtini Mponya
alipowambwa,
Mwana wa Mungu!
2. Chini ya mti wenye uchungu,
ndipo nimwombapo usafi,
mara kwa damu kaniosha
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu …
3. Akaniondolea manza,
ameingia ndani mwangu,
kwani mtini amenifia.
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu …
4. Ziwa la damu ya kiasi,
linatosa makosa yote,
laniendesha wokovuni.
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu …
5. Hicho kijito chenye maji!
U tayari kuzama humo?
Humo utaona uzima!
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu …
Comments
Post a Comment