91. Ni Damu Idondokayo
1. Ni damu idondokayo
mwilini mwa Yesu,
wakosaji wakioga,
husafishwa kweli.
Bwana wangu
Mungu wangu,
u uzima wangu,
umekutana na kufa
kwa ajili yangu!
2. Ilimpatia wokovu
mwizi kule mtini;
nami nisiyemtafuta,
inanisafisha.
Bwana wangu …
3. Shaushi aliyemlinda
Yesu aliteswa,
naye akamshuhudia:
ni mwana wa Mungu!
Bwana wangu …
4. Nipe ulimi mpya Yesu
wa kukuimbia,
Babayo tutamtukuza
Jina lake pekee.
Bwana wangu …
Comments
Post a Comment