92. Ukiwa na Vichache

1. Ukiwa na vichache 

   umtolee Bwana,

   kwani akiba yako ataiongeza.

   Vipaji vyako haba Yeye hakatai,

   kidogo kwako wewe,

   kwake kitazidi!


2. Vile vile na moyo 

   umtolee Bwana!

   Ndivyo vipaji vyema

   vinavyompendeza. 

   Kwani sisi wenyewe 

   alitukomboa,

   akiuawa Yeye 

   kwa kuwambwa mtini.


3. Ukiwa na ubaya

   umwambie Bwana! 

   Ukishindana nao, atakutakasa.

   Damu aliyotoa, ndiyo itoshayo, 

   kuosha wakosaji, 

   hata wewe vivyo.

 

4. Vitu vya mali nyingi 

   umtolee Bwana! 

   Alitoka mbinguni 

   kusumbuka hapa. 

   Alikufa mwenyewe 

   kwa ajili yako, 

   nawe hutoi chako 

   kwa ajili yake?

 

5. Wakristo na tutoe 

   shukrani kwa Mungu. 

   Hiyo ndiyo shukrani

   ya wokovu wetu. 

   Injili yake Kristo, ienee pote!

   Kwa ushuhuda wetu 

   watu waokoke. 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya