95. Bwana Yesu Alikufa

1. Bwana Yesu alikufa 

   kwa sababu yetu sisi, 

   alipata duniani 

   maumivu mengi sana.


2. Bustanini akiomba 

   akafadhaika kabisa. 

   Jasho lake kama damu 

   nchini ikadondoka.


3. Wayuda wakamwendea, 

   wakamshika, wakamfunga.

   Na rafiki zake wote 

   wakimbia, wakamwacha.


4. Na wale wakampeleka barazani

   kumhukumu. Wamhukumu yule

   mfalme, atakayewahukumu.


5. Wakamfyoza, wakampiga,

   wakampeleka Golgota. 

   Pale wakamwamba mtini,

   kwa misumari kumkaza.


6. Kukawa na giza huko,

   nchi ikatetemeka.

   Watu walioko wote, 

   Wakaona woga mwingi.


7. Na saa tisa ikifika,

   Yesu apaza sauti kuu,

   kwamba:  Yamemalizika; 

   mara akakata roho.


8. Askari wakamwendea,

   wakamwona amekufa.

   Nao wakamchoma mkuki;

   ukapenya moyo wake.


9.  Damu yake ikatoka, 

    yakatoka maji tena.

    Maji, damu iwezayo 

    kuosha uchafu wote.


10. Na watu wema wamshusha,

    wamfunga katika sanda,

    wakamweka kaburini,

    na penye mlango jiwe kuu.


11. Siku ya tatu atoka 

    Yesu Kristo kuzimuni,

    alivyotanganza kwanza.

    Yu mzima hata milele! 

Comments

Popular posts from this blog

18. Umati wa Yesu

2. Hosiana, Mesiya