96. Wakristo Twabeba Nini?
1. K: Wakristo twabeba nini?
W: Msalaba wake Yesu;
Twaenda
twashutumiwa.
2. K: Wakristo twavaa nini?
W: Twavaa vazi la Yesu;
Twaenda twashutumiwa.
3. K: Wakristo twaenda wapi?
W: Twaenda njia ya Yesu,
Ni njia yenye mateso.
4. K: Mwokozi twamwona
pale,
W: Ateswapo Goligota;
Kwa uchungu anapita
5. K: Wakristo tuvumilie
W: Njia hii yenye shida.
Mwisho wake
tutashinda.
6. K: Tushinde kwa nguvu
gani?
W: Yesu ni ushindi wetu.
Katoa ahadi kwetu.
7. K: Mwokozi wetu
kashinda
W: Mauti nalo kaburi.
Yu hai hata milele.
Comments
Post a Comment