98. Mungu Ameona Tulivyo
1. K: Mungu ameona
W: Tulivyo huku chini,
K: Neno hilo jema
W: Litokalo mbinguni
/: Ya kwamba Yesu kaja
na kutuongoza,
tufike uzimani. :/
2. K: Hujui njia
W: Uende upande gani
K: Nuru yake Bwana
W: Huangaza njiani.
/: Ya kwamba Yesu …
3. K: Kweli, unajua,
W: Mtu wa duniani.
K: Atakuongoza
W: Upate kuamini.
/: Ya kwamba Yesu …
4. K: Njooni tufungue
W: Milango ya moyoni
K: Neno lake Bwana
W: Likaingie ndani.
/: Ya kwamba Yesu …
Comments
Post a Comment